Ekwisi

Ekwisi (Italia ya Kati, 490 hivi - Amiterno, L'Aquila, Italia, 570 hivi) alikuwa mmonaki ambaye kwa utakatifu wake alieneza sana maisha ya kitawa sambamba na Benedikto wa Nursia [1].

Papa Gregori I alitangaza sifa zake akisema kila alipofika aliwafungua watu chemchemi ya Maandiko Matakatifu [2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Agosti[3].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91219
  2. Dialogues (I,4 in PL, LXXVII, coll. 165-77)
  3. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search